Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:32

Utawala wa kijeshi Guinea wamshutumu rais wa jumuiya ya ECOWAS

Wakuu wa nchi za ECOWAS na wawakilishi wengine wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa tano wa jumuiya hiyo mjini Accra, Ghana, Ijumaa Machi 25, 2022.
Wakuu wa nchi za ECOWAS na wawakilishi wengine wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa tano wa jumuiya hiyo mjini Accra, Ghana, Ijumaa Machi 25, 2022.

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umemshutumu rais wa jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwa "uongo" kutokana na wito wake wa kuiwekea vikwazo Conakry, kama itajaribu kuongeza kipindi cha mpito cha miaka mitatu kabla ya kurejesha utawala wa kiraia.

Taifa hilo maskini lakini lenye utajiri wa madini limekuwa likitawaliwa na jeshi tangu mapinduzi ya septemba 2021 yaliyomuondoa madarakani rais Alpha Conde tangu mwaka 2010.

"Uongo na vitisho vinarudisha nyuma hatua ambazo zinavunja heshima za Mkuu wa ECOWAS, Umaro Sissoco Embalo, na wakati huo huo kuchafua taswira ya ECOWAS," Kanali Amara Camara, kiongozi mwandamizi wa baraza la kijeshi, alisema katika video iliyopokelewa na shirika la habari la AFP.

Wakati wa ziara yake nchini Guinea, Embalo alisema amepata makubaliano na utawala wa kijeshi ili kutoa nafasi kwa raia waliochaguliwa baada ya miaka miwili, jambo ambalo Camara alilielezea kama "uongo".

Miaka mitatu madarakani kabla ya kurejea kwa utawala wa kiraia "haikubaliki kwa ECOWAS," Embalo, ambaye pia ni rais wa Guinea-Bissau, alisema Jumatano.

XS
SM
MD
LG