Wanahabari wa Marekani wanakabiliwa na tishio jipya ikiwemo kushambuliwa na polisi, mashambulizi ya kimitandao, ghasia pamoja na kupelekwa mahakamani, kulingana na ripoti Kamati ya Kulinda Wanahabari ya CPJ, yenye makao yake mjini New York.
Ripoti hiyo ni imefuatilia matukio tangu 2020. Katherine Jacobsen ambaye ni mratibu wa CPJ hapa Marekani, Canada na Caribbean, ameambia VOA kwamba, “Kulikuwa na matumaini mwanzoni wa utawala wa Biden, kwamba hali ungekuwa salama kwa wanahabari. Hata hivyo hali haijabadilika, wakati matukio mabaya zaidi yakiendelea kushuhudiwa.”
Kufikia Septemba mwaka huu, mashambulizi dhidi ya wanahabari hapa Marekani wakati wakifanya kazi yao yaliongezeka kwa zaidi ya asilimia 50 kulinganishwa na mwaka uliopita. Ingawa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipoteza kwenye uchaguzi wa 2020, ripoti hiyo inasema kuwa misimamo yake huenda imechangia mazingira hatari kwa wanahabari kote nchini.
Forum