Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 05:21

UNHCR yaitaka Hispania kutokiuka mkataba wa Geneva wa wakimbizi


Wahamiaji wa kiafrika katika jaribio la kuingia maeneo ya Ceuta na Melilla, October 15, 2014.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR linaihimiza Hispania kutoidhinisha pendekezo la kuwarudisha mara moja watu wanaojaribu kuingia katika maeneo inayomiliki ya Ceuta na Melilla huko Afrika kaskazini. UNHCR inaeleza kuwanyima watu haki zao za kuomba hifadhi ya kisiasa kutaisababisha Hispania kukiuka Mkataba wa Geneva juu ya wakimmbizi wa mwaka 1951.

Ripoti yake inaeleza kwamba UNHCR inasisitiza kwamba watu wanaotafuta usalama wa kimataifa wanalazimika kupata fursa ya kusikilizwa na madai yao ya kuomba hifadhi yanabidi kutathminiwa na maafisa husika. Shirika hilo linaeleza haki hii ya msingi iko hatarini kutokana na pendekezo la Hispania la kuwarudisha mara moja watu wasiokuwa na hati halali pale wanapojaribu kuvuka senyeng’e ili kuingia katika maeneo inayomiliki huko Morocco ya Ceuta na Melilla.

Miji hiyo miwili ya Hispania ni ardhi pekee inayopakana kati ya Umoja wa ulaya na Afrika. Msemaji wa UNHCR, William Spindler alisema kumekuwepo na ongezeko la idadi ya watu wanaowasili mara kwa mara kupitia njia hiyo tangu mwaka 2013.

Wahamiaji wakishikiliwa katika kituo cha muda Melilla, Machi 18, 2014.
Wahamiaji wakishikiliwa katika kituo cha muda Melilla, Machi 18, 2014.

Spindler alisema kumekuwepo na ongezeko katika kiwango cha watu wanaoingia Ceuta na Melilla kutokea nchi zinazokumbwa na vita, ghasia na mateso. Alisema asilimia 60 ya watu hao ni kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Jamhuri ya Afrika ya kati na Syria.

Alisema mwaka 2013 kiasi cha watu 4,200 waliingia maeneo hayo kwa njia zisizo halali kupitia nchi kavu au baharini.

Mwaka huu alisema zaidi ya watu 5,000 wamewasili. Idadi hii inajumuisha pia watu 2,000 wanaokimbia mgogoro wa Syria wengi wao wanawake na watoto. Lakini msemaji wa UNHCR anaiambia Sauti ya Amerika sio watu wote wanaowasili wanaonekana kuwa wakimbizi. Anasema kwamba wengi wanafanya safari kwa sababu za kiuchumi.

Pia alieleza kuwa Hispania ni sehemu ya Mkataba wa wakimbizi wa mwaka 1951. Kutokana na hilo alisema serikali lazima ifuate sheria ya kimataifa ya kuwaruhusu watu kuelezea kesi zao kwa ajili ya hifadhi. Watu ambao wanastahiki kuwa na haki ya ukimbizi, alisema lazima wapatiwe usalama wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG