Upatikanaji viungo

Mawaziri wa nchi za nje wa umoja wa ulaya wamekutana Jumatatu mjini Brussels, Ubelgiji kuijadili Burundi.

Mjadala huo ulihusu hatma ya ushirikiano kati ya nchi za umoja huo na Burundi inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa.

Umoja wa Ulaya umekuwa ukitishia kuweka vikwazo dhidi ya serikali ya Burundi kwa tuhuma kwamba imeshindwa kuheshimu haki za binadamu.

Vilevile umoja huo umekuwa ukiitaka serikali ya Burundi kufanya mazungumzo na wapinzani wake ili kumaliza tofauti zao kwa amani.

Waziri wa Burundi wa maswala ya nchi za nje Allain Nyamitwe amesema kuwa ana matumaini Umoja wa Ulaya hawataweka vikwazo kwani wamepiga hatua katika kuheshimisha haki za binadamu wakati huu.

XS
SM
MD
LG