Mkuu wa sera kuhusu hali ya hewa, wa Umoja wa Ulaya, Frans Timmermans, amesema hayo katika kongamano la 27 kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa COP27, katika mji wa El-Sheikh, Misri.
Ameongezea kwamba Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Denmark pia zimetangaza kuchangia pesa, na kwamba nchi nyingine zinaweza kuungana nao.
Amesema kwamba pesa hizo ni hatua ya mwanzo kuisaidia Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Umoja wa Mataifa utatoa Euro milioni 60 kugharamia hasara ambayo imeletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, na mikakati itawekwa namna ya kuzuia hasara katika siku zijazo.