Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 12:57

Umoja wa Mataifa yatoa ripoti ya maji.


Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- Moon
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- Moon

Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba mataifa yamefikia hatua muhimu ya malengo ya miaka mitano ya millennium kabla ya tarehe iliyopangwa

Licha ya kuwepo na taarifa nzuri kwamba mamilioni ya watu sasa wanauwezo wa kupata maji safi , ripoti mpya inaeleza kuwa utashi mkubwa wa maji unatishia malengo ya maendeleo.

Mabadiliko ya matumizi, mahitaji makubwa ya chakula, ongezeko la watu na kupanuka kwa miji ni miongoni mwa mambo yaliyopatikana katika ripoti iliyotolewa na shirika la UNESCO lenye makao yake mjini paris.

Utafiti huo sio onyo la kwanza la maji. Lakini Ulcay Unver ambaye aliratibu ripoti hiyo amesema masuala ya maji yanaonekana kuzingatiwa kidogo.

Wiki iliyopita umoja wa mataifa ulitangaza kwamba mataifa yamefikia hatua muhimu ya malengo ya miaka mitano ya millennium kabla ya tarehe iliyopangwa kupunguza idadi ya watu wnaokabiliwa na tatizo la kupata maji safi ya kunywa.

Ripoti hiyo imegundua kwamba matumizi mengine ya maji yana matatizo makubwa. Kwa mfano miundo mbinu ya hifadhi za maji, imeshindwa kwenda sambasamba na kupanuka kwa miji. Wakulima wanatumia maji zaidi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na ongezeko la watu wanaokula nyama kwa wingi. Kati ya muongo mmoja ripoti hiyo inasema dunia itahitaji asilimia 70 ya maji zaidi kuliko inavyotumia sasa.

Umoja wa mataifa unakadiria kwamba misukumo hii ya ushindani itazorotesha uchumi na mizozo miongoni mwa watu na maeneo.

XS
SM
MD
LG