Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 12:48

Uganda yatarajia ufadhili kutoka EU kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta


Majaribio ya uchimbaji wa mafuta kwenye ziwa Albert, magharibi mwa Uganda. Picha ya AP

Kampuni ya taifa ya mafuta ya Uganda (UNOC) inatarajia kupata ufadhili wa dola bilioni 5 hapo mwakani kwa ajili ya ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi, mradi uliokuwa unapingwa na EU, mkurugenzi mtendaji wa UNOC ameiambia Reuters leo Alhamisi.

“Bado hatujafikia makubaliano ya ufadhili kwa ajili ya mradi huo, lakini tunarajia hili litafikiwa katika robo ya kwanza ya mwaka wa 2023,” mkurugenzi mtendaji wa UNOC, Proscovia Nabbanja amesema.

Mwezi Februari, kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total Energies na mshirika wake wa China Oil Corporation 0883 HK zilisaini mkataba wa uwekezaji na Uganda na Tanzania, kuanzisha uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 10 ili kuzalisha na kusafirisha nje mafuta ghafi ya Uganda.

Sehemu ya uwekezaji huo inahusu dola bilioni 5 za bomba la mafuta, mradi uliokosolewa na Umoja wa Ulaya na kupitisha azimio linalolenga kuchelewesha mradi huo, ambao utaisaidia Uganda kusafirisha mafuta ghafi kwenye masoko ya kimataifa kupitia bandari moja ya huko Tanzania.

Azimio hilo la EU linaonya kuwa bomba hilo la mafuta pamoja na ujenzi wa miundo-mbinu inayohusiana na mradi huo, litasababisha kuhamishwa kutoka makazi yao karibu watu 100,000, kuhatarisha rasilimali za maji na kuhatarisha maneo ya baharini yanayolindwa huko Tanzania

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG