Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:52

‘Tuhuma binafsi dhidi ya Trump si hatari kwa usalama wa taifa’


Nancy Pelosi kiongozi wa walio wachache katika baraza la wawakilishi.
Nancy Pelosi kiongozi wa walio wachache katika baraza la wawakilishi.

Pelosi amewatahadharisha waadishi akisema haya anayozungumza ni kwa kipimo chake mwenyewe na hayatokani na muhtasari wowote wa kipelelezi alioupokea

Kiongozi wa walio wachache bungeni wa chama cha Demokratik, Nancy Pelosi amesema Jumatano madai yeyote kuhusu fedha au tuhuma binafsi dhidi ya rais mteule, Donald Trump “haziwezi kuhatarisha usalama wa taifa la Marekani.”

Lakini Pelosi alisita kueleza zaidi juu ya habari za hivi karibuni zilizojitokeza zikidai ushirikiano uliopo kati ya Russia na Trump, akisisitiza kuwa taarifa hizi zimekuwa zikizunguka kati ya waandishi kwa muda sasa lakini zilikuwa hazijathibitishwa.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema alikuwa na wasiwasi juu ya mwenendo wa rais mteule katika kuendeleza ushirikiano wa Marekani na Russia. “Nilikuwa siku zote najiuliza kitu gani ambacho Russia wanakihodhi dhidi ya Donald Trump?” aliwaambia waandishi wa habari.

Pelosi amewatahadharisha waaddishi akisema haya anayozungumza ni kwa kipimo chake mwenyewe na hayatokani na muhtasari wowote wa kipelelezi alioupokea. Kiongozi huyo wa walio wachache bungeni alijizuia kutabiri matokeo ya madai hayo yaliyoenea iwapo yatabainika kuwa kweli.

'Kompromat'

Nyaraka kama hizi za uchafuzi, zinajulikana Russia kama “kompromat” mara nyingi hutengenezwa na baadhi ya mashirika ya kipelelezi kutoa habari hasi kama uvumi ili kumchafua mtu na pengine kumlazimisha kusalimu amri.

“Hili lisiwe jambo la kumshangaza mtu yeyote kwamba Russia kila siku wanatafuta dosari ya mwanasiasa yeyote,” mwakilishi na mwenyekiti wa Kamati ya usalama ykatika bunge, Devin Nunes aliwaambia waandishi.

“Siwezi kuharakisha kutoa majumuisho yoyote. Hili pengine limekwenda nje ya maudhui,” aliongeza kusema Nunes, ni mrepublikan ambaye amewahi kufanya kazi na timu ya mpito ya Trump.

Idara za upelelezi za Marekani imehitimisha kuwa rais wa Russia, Vladimir Putin aliagiza majasusi wake kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kwa lengo la kuvuruga kampeni za aliyekuwa mgombea wa Demokratik, Hillary Clinton na kumsaidia Trump kushinda uchaguzi. Trump alishinda katika kura za wajumbe (Electoral College).

Trump alikiri katika mkutano wake na wana habari kuwa Russia iliingilia kati uchaguzi, ambaye atachukua madaraka Januari 20 kwa kipindi cha miaka minne katika Ikulu ya White House.

XS
SM
MD
LG