Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 03:09

Time Magazine yawatuza wanaopigana dhidi ya Ebola


Time Magazine yawatuza wanaopambana na Ebola

Jarida la Marekani Time Magazine limetaja “Mtu Mashuhuri wa Mwaka” katika uteuzi wake wa kila mwaka, kwa kujumlisha wote wanaopambana na ugonjwa hatari wa Ebola.

Mhariri wa Jarida hilo Nancy Gibbs alisema Jumatano kuwa madaktari hao wote na wauguzi walijitolea kupambana na “vita.”

Alisema walifanya jitihada kubwa,wakionyesha moyo wa huruma na kuhatarisha maisha yao wenyewe ili kuokoa maisha ya wengine huku wengine wao wakiambukizwa Ebola.

Gibbs alisema watoa huduma za afya wametoka katika kila pembe ya dunia, ikiwa ni pamoja na shirika la madaktari wasio na mipaka (Doctors Without Borders) na kundi la Kikristo linalotoa msaada wa afya Samaritan Purse.

Baadhi ya wafanyakazi walionusuruka kifo baada ya kuambukizwa Ebola, waliliambia Jarida hilo kuwa Mungu amewapa nafasi kuendelea kusaidia wengine.

XS
SM
MD
LG