Shambulio la kombora la Russia leo Jumanne liliuwa watu wasiopungua wanne katika mkoa wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine, maafisa wamesema. Gavana wa Kharkiv Oleh Syniehubov, alisema kwenye mtandao wa Telegram kwamba kombora hilo lilipiga sehemu ya kati ya mji wa Izyum na pia kuwajeruhi watu 20.
Syniehubov alisema shambulio hilo liliharibu jengo la makaazi la ghorofa tano pamoja na majengo kadhaa ya utawala. Mapema Jumanne, maafisa wa Ukraine walisema mashambulizi ya usiku kucha ya ndege zisizokuwa na rubani za Russia yaliharibu nyumba na majengo mengine katika mikoa kadhaa.
Jeshi la Ukraine limesema ulinzi wake wa angani ulitungua ndege 37 kati ya 65 zisizokuwa na rubani ambazo vikosi vya Russia vilirusha katika mashambulizi hayo, huku mashambulizi yakifanyika katika mikoa ya Cherkasy, Chernihiv, Kyiv, Poltava na Sumy.
Forum