Msemaji wa Kremlin Dimytry Peshkov wakati akizungumza na wanahabari amemesema kwamba maneno ya pongezi hayawezi kufikiriwa kamwe kutokana na sera zisizo za kirafiki za Marekani.
Marekani imekuwa ikipinga vikali uvamizi wa Russia nchini Ukraine wakati ikituma silaha pamoja na kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine huku ikiwa kwenye mstari wa mbele kuiwekea vikwazo. Rais wa Russia Vladimir Putin katika miaka ya nyuma ametuma ujumbe wa pongezi kwa viongozi wa Marekani kama vile Donald Trump na Barack Obama.
Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy kwa upande wake ametuma ujumbe wa heri njema kwa rais Joe Biden pamoja na watu wa Marekani wakati huu wa maadhimisho ya uhuru.
Facebook Forum