“Hakuna mahali kwa kufanya vurugu za kisiasa Marekani,” Rais Biden aliuambia mkutano wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vya watu Weusi (HBCU), akiwa mjini Philadelphia, Jumatatu.
Amesema ndani ya Marekani, kuna usuluhishaji wa tofauti zetu kwa amani kwa kutumia sanduku la kura, lakini sio wa mtutu wa bunduki. Rais Biden amesisitiza kwamba Marekani iliteseka mara nyingi na mikasa ya mauaji ya bunduki na kwamba njia hiyo haisuluhishi chochote zaidi ya kusambaratisha nchi.
Maoni ya Biden yametolewa takriban saa 24 baada ya maafisa wa idara ya ulinzi wa viongozi ya Marekani, kumwona mtu anayeshukiwa kuwa na bunduki kwenye uwanja wa gofu wa Rais mstaafu Donald Trump, West Palm Beach, Florida.
Forum