Rais wa Marekani Barack Obama amekutana leo Jumatano, na mfalme Salman wa Saudi Arabia huku kukiwa na mahusiano yenye mivutano na tofauti ambazo zimejitokeza jinsi ya kupambana na ugaidi na mizozo ya kieneo.
Walikuwa na mkutano wa saa mbili kwenye Erga Palace.
Salman alimueleza Obama kuwa yeye na watu wa Saudi Arabia wamefurahishwa na ziara yake, ikiwa ni ziara ya nne ya rais wa Marekani.
amrekani na washirika wake wa kiarabu watazungumzia masuala yanayolikabili eneo hilo katika mkutano ambao utahudhuriwa na washirika sita wa GCC ya mataifa ya ghuba, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Bahrain na Oman.