Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:56

Rais Obama akutana na mwana mfalme wa Abu Dhabi


Rais wa Marekani Barack Obama akizungumza na mwana mfalme wa UAE Mohammed bin Zayed Al Nahyan huko White house.
Rais wa Marekani Barack Obama akizungumza na mwana mfalme wa UAE Mohammed bin Zayed Al Nahyan huko White house.

UAE na Qatar ni nchi mbili pekee za Mashariki ya Kati zinazosaidia NATO katika hatua zake za kijeshi dhidi ya kanali Moammar Gadhafi.

Taarifa ya White House baada ya mazungumzo hayo inaeleza kwamba viongozi hao wawili walijadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya Mashariki ya Kati na yalikuwa majadiliano yenye manufaa, lakini haikutoa maelezo zaidi.

Kwa upande wake shirika la habari la Emirates lilitowa maelezo zaidi likiripoti kwamba mazungumzo yalihusu msaada unaotolewa na Umoja wa Nchi za Karabu UAE, kwa NATO katika hatua zake za kijeshi nchini Libya na juhudi za kuzuia kuenea kwa siasa kali.

UAE na Qatar ni nchi mbili pekee za Mashariki ya Kati zinazosaidia NATO katika hatua zake za kijeshi dhidi ya kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi. UAE imepeleka pia polisi kuisaidia Bahrain kuzima maandamano ya upinzani mwezi uliyopita.

Umoja wa Falme za Kiarabu umekua kisiwa cha utulivu na usalama katika Mashariki ya Kati inayokumbwa na misukosuko.

Lakini makundi ya haki za binadamu yanasema serikali ya taifa hilo la kifalme imekuwa ikizima sana upinzani wowote ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa wanaharakati watano wa mtandao wanaotaka mageuzi. Wanabloga hao walitia saini pendekezo kwenye mtandao linalodai mageuzi ya kisiasa.

XS
SM
MD
LG