Maelfu ya raia wa Argentina waliingia katika mitaa ya Buenos Aires siku ya Jumatano kupinga amri ya mageuzi ya kiuchumi na kupunguza udhibiti uliopendekezwa na Rais Javier Milei.
Wakiandamana kwa amri ya vyama vya wafanyakazi, waandamanaji hao waliitaka mahakama kuingilia kati ili kubatilisha uamuzi huo ambao wanasema utawaondoa wafanyakazi pamoja na ulinzi kwa mnunuzi.
Bunge katika kikao chake kisicho cha kawaida wiki hii, kwa ombi la Milei, aliyekuwa ofisini tangu Desemba 10 ili kuufikiria mpango huo. Amri hiyo itabadilisha au kufuta zaidi ya kanuni 350 za kiuchumi katika nchi iliyozoea kuingilia kati kwa serikali katika soko.
Forum