Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 03:01

Radi yaua watoto 18 Uganda.


Watoto wa shule Uganda wakicheza ngoma.

Watoto 18 wapoteza maisha na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika mfululizo wa radi mbaya huko nchini Uganda ambapo wataalam walauimu majengo kukosa kinga.

Vyombo vya habari nchini Uganda vimesema radi imeuwa watoto 18 katika shule moja ya msingi magharibi mwa nchi hiyo jumanne, ikiwa ni mfululizo wa matukio ya karibuni ya radi mbaya nchini humo.

Gazeti linalomilikiwa na serikali ya Uganda la New Vision limesema wanafunzi hao walikufa papo hapo wakati walipokuwa wakisubiri mvua na dharuba kumalizika katika shule ya msingi ya Runyanya katika wilaya ya Kiryandongo kaskazini mwa mji mkuu Kampala. Gazeti hilo pia limesema watu 36 walijeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ilitokea kiasi cha muda wa saa 10:30 jioni kwa saa za Uganda.

Gazeti hilo pia linaripoti kuwa radi nyingine ilipiga na kujeruhi watoto 37 na walimu wawili katika shule moja ya msingi katika wilaya ya kaskazini ya Zombo nchini humo jumanne.

Ripoti hiyo inasema radi imeuwa zaidi ya watu 40 huko Uganda katika wiki za karibuni. Wataalamu wanasema ukosefu wa waya za kuzuia radi kwenye majengo mengi ya Uganda huenda ikawa ni chanzo cha idadi kubwa ya majeruhi nchini humo.

XS
SM
MD
LG