Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:07

Papa Francis apokelewa kwa shangwe Philippines


Papa Francis akiwasili mji mkuu wa Philippines, Manila, Alhamisi ya Januari15, 2015.
Papa Francis akiwasili mji mkuu wa Philippines, Manila, Alhamisi ya Januari15, 2015.

Kiongozi wa Kanisa la Roman Katoliki , Papa Francis Alhamisi alipokelewa kwa furaha nchini Philippines, kuanza ziara yake ya siku tano.

Ziara yake hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu katika nchini humo, ambapo Philippines, ndiyo nchi yenye waumini wengi wa kanisa Katoliki, barani Asia.

Kengele za makanisa zilisikika nchini nzima wakati kiongozi huyo alipokuwa anaelekea makao mji mkuu wa Manila, mara baada ya kutembelea nchi ya Sri Lanka.

Halaiki kubwa ya watoto wa shule walicheza na kuimba wakati akiteremka katika ndege na kusalimiana na Rais wa Philippines, Benigno Aquino.

Maelfu ya watu walipanga foleni katika mitaa ya Manila, na kumshangilia kiongozi huyo wakati msafara wake ulipopita.

Akiwa safarini, Papa Francis, alizungumza na wanahabari kuhusu shambulizi la ugaidi la wiki iliyopita nchini Ufaransa.

Papa ametetea uhuru wa kujieleza kama jambo muhimu kwa haki za binadamu, lakini akasema huwezi kudhihaki ama kutukana imani za wengine.

XS
SM
MD
LG