Upungufu wa chakula na kuendelea kwa hali ya ukame huko Kenya kumeanza kusababisha vifo miongoni mwa wakazi wa majimbo ya kaskazini mashariki, pwani na majimbo ya kati na mashariki.
Katika sehemu za kaskazini mashariki watu kadhaa wamekufa na maisha ya mamia ya wengie yamo hatarini kwa ukosefu wa chakula maji na huduma za afya.
Katika maeneo ya Pokoto, Baringo na Turkana, hali inaripotiwa kuendelea kuwa mbaya zaidi na baadhi ya hospitali hazina maji au dawa kuweza kutoa matibabu.
Mfanayakazi wa hopitali moja huko Baringo anasema "kutokana na ukosefu wa maji wagonjwa hawawezi kumeza dawa, na huwezi kumpiga mtu shindano ikiwa huna maji".
Hali hii yote inatokea wakati wanasiasa wanavutana kwajili ya nyadhifa za serikali au kujitayarisha kwaajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani.
Hata hivyo waziri mkuu Riala Odinga ametembelea baadhi ya maeneo yanayoathirika sana na hali ya njaa, ili kuwaelezea wakazi juu ya mipango ya serikali ya kuwasaidia kwa chakula.