Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 11:11

Polisi wa Nigeria washutumiwa kwa mauaji holela


Jeshi la polisi nchini Nigeria

Mkuu wa polisi nchini Nigeria Mohammed Abubakar anasema idara yake inashutumiwa kwa mauaji ya watu wasio na hatia

Mkuu mpya wa polisi nchini Nigeria anasema kwamba polisi mara kwa mara wanafanya mauaji kwa watu wasio na hatia huko jela na kuwadai rushwa.

Katika hotuba yake ya Jumatatu huko Abuja, kaimu mkuu wa jeshi la polisi, Mohammed Abubakar, alisema jeshi la polisi lilishuka kiwango chake cha kazi.

Mkuu huyo mpya alisema kitengo cha polisi cha kupambana na uhalifu kimekuwa “timu ya mauaji” na watu wasio na hatia wanawekwa jela kwa sababu hawana uwezo wa kulipa dhamana haramu. Aliagiza wale waliokamatwa kinyume cha sheria waachiwe huru, na kuvunja vizuizi vya barabarani ambavyo wa-Nigeria wengi wanaviangalia kama vituo vya kukusanyia rushwa.

Akizungumza na kundi la polisi na maafisa wa usalama, Abubakar aliahidi mabadiliko makubwa ya kuzungumzia utovu wa nidhamu na kurudisha imani ya umma katika jeshi la polisi.

Rais Goodluck Jonathan alimteua Abubakar, mwezi uliopita baada ya kuwalazimisha mkuu wa zamani wa polisi na wasaidizi wake wa juu kustaafu. Rais amekuwa chini ya shinikizo kali la kusitisha mashambulizi yanayofanywa na kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Boko Haram.

Jumanne, mabomu mawili yalilipuka katika mji wa kaskazini wa Kaduna na kumuuwa mfanyakazi mmoja wa kitengo cha kutegua mabomu wakati akijaribu kutegua moja ya mabomu hayo. Hakukuwa na madai ya haraka ya nani aliyehusika na milipuko hiyo.

Boko Haram lilidai kuhusika na mashambulizi kama hayo huko Kaduna mwanzoni mwa mwezi huu. Kundi hilo linalaumiwa kwa dazeni ya vifo vinavyohusiana na mabomu na ufyatuaji risasi zaidi ya miezi 18 iliyopita, hasa huko kaskazini mwa Nigeria. Kundi hilo linasema linataka kuweka mfumo mkali wa sharia ya ki-Islam kote nchini humo.
XS
SM
MD
LG