Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 03:34

Nigeria inasema imewaokoa wanafunzi 16 waliotekwa kaskazini magharibi mwa nchi


Jimbo la Sokoto nchini Nigeria
Jimbo la Sokoto nchini Nigeria

Mateka waliookolewa wamekabidhiwa kwa serikali ya jimbo la Sokoto kwa hatua Zaidi, alisema Meja Jenerali Edward Buba.

Jeshi la Nigeria limesema Jumamosi kuwa limewaokoa wanafunzi 16 waliotekwa nyara kaskazini magharibi mwa nchi eneo ambalo limekumbwa na utekaji nyara mkubwa.

Watu wenye silaha waliwakamata wanafunzi hao siku chache baada ya utekaji nyara wa watoto 280 katika eneo hilo, ambako magenge ya uhalifu yanazilenga shule ili kudai fidia. Jeshi limesema limewaachia huru wanafunzi 16 na mwanamke mmoja siku ya Alhamisi.

Kundi hilo lilitekwa nyara katika jimbo la Sokoto hapo Machi 9. “Mateka waliookolewa wamekabidhiwa kwa serikali ya jimbo la Sokoto kwa hatua Zaidi”, alisema msemaji Meja Jenerali Edward Buba. Hakutoa maelezo zaidi kuhusu operesheni hiyo.

Wakati wa shambulio dhidi ya seminari ya Kiislamu katika wilaya ya Gada, wafanyakazi waliliambia shirika la habari la AFP kuwa watu hao wenye silaha waliwazingira wanafunzi walipokuwa wamelala nje.

Mwanamke huyo alitekwa nyara katika sehemu nyingine ya wilaya hiyo. Utekaji nyara wa Sokoto ulifuatia utekaji nyara wa wanafunzi 280 uliofanywa na genge la watu katika jimbo la Kuriga, Kaduna, hapo Machi 7 ambao ulisababisha malalamiko ya kitaifa kuhusu ukosefu wa usalama nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG