Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 21:04

Netanyahu awasili Washington


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Siku mbili kabla ya hotuba yenye utata ya waziri mkuu wa Israel, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anajaribu kurekebisha uhusiano katika lengo la kuondoa mgongano wa kidiplomasia.

Waziri Kerry alikiambia kituo cha televisheni cha ABC kwamba waziri mkuu wa Israel anakaribishwa kuzungumza Marekani kwa sababu Marekani ina uhusiano wa karibu na Israel kuhusu usalama kuliko muda wowote ule.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameshawasili Washington DC.

Kabla ya kuondoka Israel, Netanyahu, alisema yupo katika ziara ya kihistoria kujaribu kuzuia makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Anatarajiwa kuhutubia mabaraza mawili ya bunge la Marekani kesho Jumanne.

Netanyahu aliishangaza Washington, mapema mwaka huu kwa kutangaza ziara yake kufuatia mwaliko wa spika John Boehner .

Hali hiyo inaonekana kama kuvunja itifaki ya kihistoria ya kuratibu ziara kama hiyo na White House.

XS
SM
MD
LG