Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 15:49

Nchi za Afrika Kaskazini zatakiwa kudhibiti mipaka yao


mpiganaji muasi akifyatua risasi hewani wakati mazungumzo ya mapatano yameanza baina ya viongozi wa kikabila na viongozi wa wa waasi katika kituo cha ukaguzi baina ya Tarhouna and Bani Walid jumanne

Wito huo uliotolewa jumatano unafuatia tukio la wiki hii ambapo baadhi ya maafisa wa Serikali iliyoondolewa madarakani ya Ghadafi waliwasili kwa msafara wa magari nchini Niger.


Marekani inazihimiza nchi za Afrika Kaskazini kudhibiti mipaka yao vyema na kuwakamata maafisa wowote kutoka Serikali ya zamani ya Libya ya Muammar Ghadaffi watakaojaribu kuingia huko.

Wito huo uliotolewa jumatano unafuatia tukio la wiki hii ambapo baadhi ya maafisa wa Serikali iliyoondolewa madarakani ya Ghadafi waliwasili kwa msafara wa magari nchini Niger.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inaeleza kwamba maafisa wa Marekani wamewasiliana na nchi za Afrika Kaskazini pamoja na zile zisizokuwa na mipaka ya pamoja na Libya, kuwahimiza kuheshimu majukumu yao ya kimataifa kwa kuwakamata maafisa wanaokimbia Serikali ya Ghadafi na kuzuia fedha zozote au mali nyingine watakazokuwa wamebeba.

Wito huo unafatia kuwasili Niger mapema wiki hii msafara wa magari uliowabeba maafisa wa kijeshi na maafisa wengine ambao walikuwa washirika wakaribu wa Ghadafi wanaokabiliwa na mashtaka ya kimataifa.

Msemaji wa wizara ya nchi za nje wa Marekani Victoria Nuland alisema kile ambacho Washington inafahamu ni kwamba msafara huo ulivuka mpaka wa kusinimagharibi mwa Libya na kuingia Niger ukiwa imebeba raia wa Libya kati ya 20 hadi 25, na ripoti za habari zinasema kuwa magari miambili yaliyohusika yalikuwa sio sahihi.

Bi Nuland alisema mbali na Niger, Marekani imewasiliana na nchi za Mali, Mauritania, Chad na Burkina faso, kuwahimiza kuheshimu maazimio ya baraza la usalama la umoja mataifa juu ya Libya na kudhibiti mipaka yao.

Bi Nulanda alisema majirani wa kaskazini wa Libya, ikiwa ni Tunisia, Algeria na Misri wamekuwa wakishirikiana na umoja mataifa kwa miezi kadhaa na kwamba wasiwasi sasa umelengwa kwenye mipaka ya kusini ambayo
Ghadafi na washirika wake wanaweza kujaribu kutumia kukimbia.

Mapema Jumatano Pentagon ilisema Marekani haina maelezo yeyote ya kuthibitisha kuwa Muammar Ghadafi ameondoka Libya.

XS
SM
MD
LG