Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 07:38

Mwanasayansi wa Sweden ashinda Tuzo ya Nobel kwa utafiti wake kutambua vinasaba vilivyotoweka


Mwanasayansi wa Sweden Svante Paabo akiwa Leipzig, Ujerumani, April 27, 2010.

Tuzo ya Nobel mwaka huu katika Tiba imetolewa kwa mwanasayansi wa Sweden kwa kuweza kutambua vinasaba vya viumbe Neanderthal, waliotoweka, ambao ni ndugu wa karibu wa wanaadamu wa leo.

Katika taarifa Jumatatu Taasisi ya Nobel ilisema Svante Paabo ametunukiwa tuzo “kwa kuanzisha muelekeo mpya wa utafiti wa historia ya mabadiliko ya maisha yetu.”

Msweden huyo mwenye umri wa miaka 67 aliweza kutatua changamoto ngumu za kiufundi za kushughulikia sampuli za kale, zilizo dhaifu na kufanikiwa kupata mtiririko wa kinasaba (genome), taasisi hiyo ilisema.

“Hili lilitekelezwa,” kulingana na taarifa hiyo, “kutokana na ugunduzi makini wa kushtua wa aina nyingine ya kinasaba (hominin) kilichotoweka, Denisova, inayotokana kikamilifu na takwimu za kinasaba (genome) kutoka katika sampuli ya mfupa wa kidole.”

Kazi yake Paabo ilithibitisha kuwa viumbe Homo sapiens, Neanderthals na Denisovans walichanganyika “ wakati wa kipindi cha kuishi pamoja,” ikipelekea kuchanganyika kwa vinasaba vya archaic katika viumbe vya hivi sasa.”

Paabo alishirikiana na Taasisi ya Max Planck For Evolutionary Anthropology, huko Leipzig, Ujerumani, na Taasisi ya Okinawa of Science and Technology, iliyoko Okinawa, Japan.

Tuzo ya Tiba ni ya kwanza kati ya tuzo nyingine tano zitakazo tolewa wiki hii, na kufikia kilele cha Tuzo ya Amani ya Nobel siku ya Ijumaa.

Tuzo ya Uchumi itafuatia Octoba 10. Ni tuzo pekee ambayo haikubuniwa chini ya usia wa muanzilishaji Alfred Nobel.

Tafrija rasmi ya Tuzo ya Nobel itafanyika Desemba huko Stockholm.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG