Polisi hao watatu walifika katika nyumba mmoja kufuatilia malalamiko ya ghasia za nyumbani katika wilaya ya Puy de Dome.
Walikuwa katika hatua ya kumokoa mwanamke mmoja na hapo ndipo waliposhambuliwa kwa bunduki na mwanaume mwenye umri wa miaka 48.
Manaume huyo alimuua polisi mmoja na kumjeruhi mwengine walipowasili kwenye nyumba hiyo majira ya saa sita za usiku.
Pia maafisa wengine wawili walipigwa risasi baadae kufuatana na afisi ya mwendesha mashtaka wa mji wa Clermont Ferrand.
Mwanamke ambaye anaripotiwa kuwa muathirika wa manyanyaso ya nyumbani alipanda juu ya paa ya nyumba kwa usalama wake kabla ya kuokolewa na polisi.