“Idadi hiyo bado inaweza kubadilika,” mwendesha mashtaka Maylis De Roeck ameliambia shirika la habari la Reuters katika ujumbe wa maandishi, akiongeza kuwa takriban watu 50 walikuwa wamejeruhiwa katika mlipuko huo, ambao uliunguza majengo kadhaa na kusababisha sehemu ya mbele ya mmoja kati ya majengo hayo kuporomoka.”
Kati ya watu wawili waliokuwa awali wanasadikiwa kutoweka, mmoja wao amepatikana akiwa hospitali na anatibiwa, mwendesha mashtaka alisema, akiongeza: “operesheni ya kumtafuta mtu wa pili inaendelea.”
Maafisa wa mji hawajatoa baado taarifa kuhusu kile kilicho sababisha mlipuko, ambapo mashuhuda walisema ulitokea baada harufu kali ya gesi katika eneo hilo.
Mlipuko huo ulipelekea matukio ya ghasia na uharibifu katika mtaa wa kihistoria wa Rue Saint Jacques, kuaanzia Kanisa la Notre-Dame de Paris hadi Chuo Kikuu cha Sorbonne, wakati watu walipokuwa wanaelekea majumbani kutoka kazini.
Pia ilibomoa eneo la mbele la jengo mmoja ambalo kuna shule ya mitindo ya Paris American Academy yenye wanafunzi wengi wakigeni.
Florence Berthout, meya wa wilaya ya Paris ambako mlipuko ulitokea, alisema wanafunzi 12 ambao walitakiwa kuwepo darasani katika shule hiyo ya academy wakati huo bahati nzuri walikuwa wamekwenda kuzuru maonyesho pamoja na mwalimu wao.
“Isingekuwa hivyo, idadi ya vifo ingekuwa ya kutisha,” Berthout alikiambia kituo cha televisheni cha BFM
Alisema watoto watatu waliokuwa wanapita njia wakati wa mlipuko huo ni kati ya wale waliojeruhiwa, japokuwa hali zao haziko hatarini.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters.
Forum