Dennis Kimetto mwanaridha kutoka Kenya amevunja rekodi za mbiyo za Marathon mjini Berlin, Ujerumani siku ya Juampili na kuwa mtu wa kwanza kukimbia mbiyo hizo kwa chini ya saa 2 na dakika tatu.
Kimetto mwenye umri wa miaka 30, alimpita Mkenya mwenzake bingwa wa mbiyo hizo Emmanuel Mutai, karibu mili tatu kabla ya kumaliza mbiyo na kuweka rikodi ya saa 2 dakika 2 sekunde 27.
Rikodi ya awali ilikua imewekwa na Mkenya mwenzake Wilson Kiplagat mwaka mmoja uliyopita huko huko Berlin, alipokimbia muda wa saa 2:03:23. Katika mbio za Jumapili Mkenya Mutai alishika nafasi ya pili akitumia mjda wa saa 2:03:13 akifuatwa na Methopia Abera Kuma aliyetumia saa 2:05:56.
Kwa upande wa wanawake Methopia Tirfi Tsegaye alinyakua ushindi akitumia muda wa 2:20:18, huku mwenzake Feyse Tadese alishika nafasi ya pili akitumia muda wa 2:20:27