Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 09:47

Mjumbe wa Marekani aelekea Sudan


Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya lori la misaada la Umoja wa Mataifa katika mji wa Kadugli, Sudan, June 9, 2011.
Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya lori la misaada la Umoja wa Mataifa katika mji wa Kadugli, Sudan, June 9, 2011.

Wizara ya Mambo ya Nje inasema Marekani inaunga mkono mazungumzo baina ya pande hizo mbili huko Addis Ababa

Mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Sudan, Princeton Lyman anaelekea Sudan kwa mazungumzo yenye lengo la kumaliza uhasama baina ya vikosi vya usalama vya kaskazini na kusini mwa Sudan wakati Kusini ikijiandaa kutangaza uhuru wake wiki ijayo.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje imesema Jumamosi bwana Lyman atahudhuria sherehe za uhuru wa Sudan Kusini Julai tisa katika mji mkuu mpya, Juba.

Taarifa zinasema Lyman atakwenda kwanza Addis Ababa , Ethiopia ambako mazungumzo baina ya kaskazini na sudan kusini yanaendelea wakati mapigano yakiwa yamepamba moto katika maeneo ya mipaka ikiwemo kusini mwa Kordofan na eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei.

XS
SM
MD
LG