Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 07, 2025 Local time: 23:04

Meli za kutegua mabomu zimewasili bahari ya Baltic


Meli ya kivita kutoka muungano wa NATO
Meli ya kivita kutoka muungano wa NATO

Meli mbili kubwa za kuondoa mabomu, kutoka Ubelgii na Uholanzi, zimewasili katika mji mkuu wa Tallinn, nchini Estonia, leo Ijumaa.

Muungano wa ulinzi wa NATO, umesema kwamba meli hiyo imeimarisha doria katika bahari ya Baltic, kutokana na migogoro ya hivi karibuni katika eneo hilo.

Usalama umeimarishwa katika bahari ya Baltic, ikiwemo ndege na meli za kijeshi pamoja na ndege zisizokuwa na rubani kupiga doria sehemu hiyo.

Meli nne kubwa za kuondoa mabomu za Nato vile vile zimeelekea katika bahari ya Baltic.

Forum

XS
SM
MD
LG