Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa siku ya Jumanne kuhusiana na shambulizi la anga la Israel siku ya jumapili lililosababisha vifo vya Wapalestina 45 waliokuwa kwenye hifadhi katika kambi ya wakimbizi huko Rafah, na kuwajeruhi wengine 200.
“Picha hizo zilikuwa za kuumiza moyo”, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller aliwaambia waandishi wa habari. Alisema wakati Israel ina haki ya kuwafuata Hamas, Israel ina wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili kupunguza madhara ya raia wakati inafanya operesheni zake.
“Tutaendelea kusisitiza kwa Israeli wajibu wao wa kuzingatia kikamilifu sheria za kimataifa za kibinadamu, kupunguza athari za operesheni zao kwa raia, na kuongeza mtiririko wa misaada ya kibinadamu kwa wale wanaohitaji”, Miller alisema, akiongeza jeshi la Israeli limeahidi uchunguzi wa haraka, wa kina, na wa uwazi. “Tutafuatilia kwa karibu matokeo hayo”, alisema.
Forum