Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 07, 2025 Local time: 12:23

Marco Rubio anakutana na maafisa wa Costa Rica na Guatemala leo Jumanne.


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio akiwa katika ziara yake la Latin Amerika. Feb. 1, 2025.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio akiwa katika ziara yake la Latin Amerika. Feb. 1, 2025.

Rubio alikuwa nchini El Salvador kwa mazungumzo na Rais Nayib Bukele na alitangaza kuwa Bukele alikubali kupokea wahamiaji kutoka Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio anapanga kufanya mikutano leo Jumanne na maafisa wa Costa Rica na baadaye nchini Guatemala kama sehemu ya ziara yake ya Latin America inayolenga uhamiaji, ushirikiano wa usalama, na kukabiliana na ushawishi wa China katika eneo hilo.

Rubio alikuwa nchini El Salvador kwa mazungumzo siku ya Jumatatu na Rais Nayib Bukele na alitangaza kwamba Bukele alikubali kupokea wahamiaji wowote kutoka Marekani, bila kujali utaifa wao.

Pia amejitolea kufanya hivyo kwa wahalifu hatari ambao kwa sasa wanashikiliwa na kutumikia kifungo chao nchini Marekani, japokuwa ni raia wa Marekani au wakazi halali, Rubio alisema. Serikali ya Marekani haiwezi kisheria kuwafukuza raia wa Marekani Kwenda kwingineko.

Rubio amesema El Salvador itashirikiana kikamilifu katika kuwarudisha nyumbani raia wa El Salvador ambao wako Marekani kinyume cha sheria akiyaita makubaliano hayo kuwa makubaliano ya kipekee, ya kihistoria katika uhamiaji popote duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG