Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 00:47

Maporomoko ya ardhi Malaysia yalisababisha vifo vya watu 31na uharibifu mwingine wa mali


Maporomoko ya ardhi huko Malaysia

Maelfu ya watu walifukiwa walipokuwa wamelala katika mahema yao kwenye shamba la Farther’s Organic huko Batang Kali eneo maarufu la mapumziko takriban kilomita 50 kaskazini mwa mji mkubwa zaidi nchini humo wa Kuala Lumpur wakati maporomoko ya ardhi yalipoikumba eneo hilo mapema asubuhi ya Desemba 16

Ripoti za awali kutokana na uchunguzi unaoendelea kuhusu maporomoko mabaya ya ardhi nchini Malaysia yaliyosababisha vifo vya watu 31 katika shamba na kambi zinaonekana kuashiria kuwa eneo hilo halikutengwa kwa matumizi ya kilimo, biashara au mapumziko afisa mwandamizi wa serikali aliiambia VOA siku ya Alhamisi.

Maelfu ya watu walifukiwa walipokuwa wamelala katika mahema yao kwenye shamba la Farther’s Organic huko Batang Kali eneo maarufu la mapumziko takriban kilomita 50 kaskazini mwa mji mkubwa zaidi nchini humo wa Kuala Lumpur wakati maporomoko ya ardhi yalipoikumba eneo hilo mapema asubuhi ya Desemba 16. Janga hilo liliitikisa nchi na kusababisha wito mpya wa kuongezwa kwa usalama na uwajibikaji.

"Eneo ambalo Shamba la Father’s Organic lilijengwa lilikuwa limeamuliwa kuwa eneo lisilofikika. Kwa hivyo maendeleo ya shamba hilo yalikuwa ni ukiukaji kwa masharti ya idhini ya ripoti ya EIA (tathmini ya athari za mazingira) iliyoidhinishwa kwa Malaysia Botanical Gardens Resort Sdn. Bhd, Wizara ya Maliasili, Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Malaysia ilisema katika taarifa iliyoandikwa Jumatatu kujibu maswali ya VOA.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG