Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu wa NBA Dikembe Mutombo, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa safu ya ulinzi katika historia ya NBA na balozi wa muda mrefu wa kimataifa wa mchezo huo amefariki dunia Jumatatu (Septemba 30, 2024) baada ya kuugua ugonjwa wa saratani ya ubongo. Alikuwa na umri wa miaka 58.
Familia yake ilieleza miaka miwili iliyopita kwamba Mutombo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alikuwa anapatiwa matibabu huko Atlanta kutokana na uvimbe kwenye ubongo. NBA ilisema alifariki dunia akiwa amezungukwa na familia yake.
Dikembe Mutombo alikuwa mkubwa kuliko maisha, Kamishna wa NBA Adam Silver alisema. Uwanjani alikuwa mmoja kati ya walinzi wakuu bora kuwahi kutokea katika historia ya NBA. Akiwa nje ya uwanja alitumia muda wake kuwasaidia wengine.
Mutombo alicheza misimu 18 kwenye ligi ya NBA, akitokea chuo kikuu cha Georgetown na alichezea timu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Denver, Atlanta, na Houston.
Mutombo alicheza mara ya mwisho msimu wa mwaka 2008-09, akitumia muda wake baada ya kustaafu kujishughulisha na masuala ya hisani na huduma za dharura. Alizungumza lugha tisa na alianzisha Wakfu wa Dikembe Mutombo mwaka 1997, akizingatia kuboresha afya, elimu na ubora wa maisha kwa watu wa Congo.
Matukio
-
Oktoba 15, 2024
Ni namna gani jamii inaangazia huduma ya kiroho katika uponyaji.
-
Oktoba 07, 2024
Mwigizaji John Amos akumbukwa kwa kazi zake
Forum