Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 22, 2025 Local time: 08:17

Kambi ya kijeshi Mali yashambuliwa na wanajeshi 17 kuuwawa


Daun-daun yang tertutup embun beku terlihat pada hari musim dingin di kota Uttenweiler-Aderzhofen, Jerman.
Daun-daun yang tertutup embun beku terlihat pada hari musim dingin di kota Uttenweiler-Aderzhofen, Jerman.

Washukiwa wanamgambo wa kiislamu wameshambulia kambi moja ya kijeshi katikati ya Mali jumanne na kuuwa wanajeshi 17. Lilikuwa tukio baya zaidi kulikumba jeshi la Mali katika shambulizi tangu januari mwaka 2012, pale makundi yenye uhusiano na Al Qaida kuteka kambi ya kijeshi katika eneo la kaskazini mwa nchi.

Jeshi linasema wanajeshi 17 waliuwawa pale washukiwa wanamgambo wa kiislamu waliposhambulia kambi ilio maeneo ya ndani katika mji wa wa Nampala nchini Mali. Wanajeshi wengine 35 walijeruhiwa pale washambuliaji walipochoma majengo, na kupora maduka na kushambulia maeneo ya wanajeshi katika kambi kilometa chache kusini mwa mpaka na Mauritania.

Shambulizi hilo lilifwatia hali ya ongezeko la ghasia katika mkoa wa kati wa Mopti ambalo linajumuisha sio tu mashambulizi kwa vikosi vya usalama lakini pia mapambano baina ya wanamgambo na makundi yenye silaha dhidi ya ardhi.

Hali hiyo imezidi kuzorota tangu mwaka 2015 hususan kwa ajili ya kutekuwepo kwa serikali katika baadhi ya maeneo ya eneo hilo anasema Boukary Sangare, mtafiti ambaye amekuwa akifwatilia mzozo katika eneo la kati kwa mwongo mmoja sasa.

Mali inahitaji haraka kushughulikia mizozo inayosambaa katika eneo la kati. Lakini tume ya umoja mataifa ya ulinzi wa amani tayari wanafanya kazi nyingi upande wa kaskazini na vikosi vya ufaransa kwenye operesheni ya Barhane wanajihusisha na makundi ya kigaidi katika maeneo ya kaskazini, na raslimali ziko haba.

Kaneli wa jeshi kaneli meja Abdrahamane Baby anasema, Mopti siyo eneo jipya, lakini tunakabiliana na vitisho vipya katika eneo kutoka katika makundi ya kigaidi ambayo hayajatia saini makubaliano ya amani. Tishio kubwa la usalama bado liko kaskazini mwa Mali. Kile tunachokiona katika eneo la kati, kinatokana na mizozo ya kaskazini.

Siku ya Jumanne makundi mawili yenye silaha yalidai kuhusika na shambulizi la Nampala. Kituo cha redio kilipokea simu kutoka kwa ushirika wakitaifa katika ulinzi wa watu wa Peul National Allaince for the safeguarding of Peul identity na Restoration of Justice, kundi la wanamgambo kutoka kabila la Peul. Hii itakuwa mara ya kwanza kundi hilo ambalo lilianzishwa mwezi ulopita na linajumuisha baadhi ya wale walopigana pamoja na wanamgambo wa kiislamu, ndio walofanya shambulizi hilo.

Shambulizi hilo la Nampala ni baya sana kuwahi kulikumba jeshi la Mali tangu shambulizi kama hilo hapo mwaka 2012, pale wapiganaji wa Ansar Dine na makundi yenye uuhusiano na Al Qaida walipoteka kambi ya jeshi huko Aguelhok kaskazini mwa Mali

XS
SM
MD
LG