Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 01:04

Mahakama ya Kikatiba Madagascar yamtangaza Andry Rajoelina kuwa mshindi wa uchaguzi

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina akiwasalimu wafuasi wake huko Antananarivo, Novemba 3, 2018. REUTERS/Malin Palm
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina akiwasalimu wafuasi wake huko Antananarivo, Novemba 3, 2018. REUTERS/Malin Palm

Mahakama ya Kikatiba ya Madagascar siku ya Ijumaa ilimtangaza Rais aliye madarakani Andry Rajoelina kuwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi uliopita, na hivyo kumpa muhula mwingine wa tatu.

Mahakama ya Kikatiba ya Madagascar siku ya Ijumaa ilimtangaza Rais aliye madarakani Andry Rajoelina kuwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi uliopita, na hivyo kumpa muhula mwingine wa tatu.

Rajoelina alipata asilimia 58.96 ya kura zilizopigwa, mahakama ilisema baada ya kutupilia mbali changamoto mbalimbali zilizowasilishwa dhidi ya matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi.

Andry Rajoelina amechaguliwa kuwa rais wa jamhuri ya Madagascar na anachukua madaraka yake punde tu atakapoapishwa, alisema Florent Rakotoa-risoa, mkuu wa mahakama ya kikatiba.

Mojawapo ya changamoto ambazo zilitupiliwa mbali ni pamoja na moja kutoka kwa mshindi wa pili, mbunge Siteny Randriana-soloniaiko, ambaye alipata asilimia 14.39 ya kura kwa mujibu wa mahakama.

Forum

XS
SM
MD
LG