Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:47

Mahakama ya ICC kuchunguza uhalifu Ivory Coast


Maiti za watu wasiotambulika zikizikwa katika makaburi ya pamoja mjini Abidjan, Aprili 15, 2011.
Maiti za watu wasiotambulika zikizikwa katika makaburi ya pamoja mjini Abidjan, Aprili 15, 2011.

Luis Moreno -Ocampo kuchunguza visa vya uhalifu Ivory Coast

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya jinai amewasili nchini Ivory Coast kuchunguza visa vya uhalifu vilivyotendwa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Mwendesha mashitaka huyo Luis Moreno- Ocampo alikutana kwa muda mfupi na Waziri Mkuu Guillaume Soro baada ya kuwasili nchini humo Ijumaa jioni. Bwana Ocampo anasema atakutana na maafisa wa Ivory Coast pamoja na waathiriwa wa mtafaruku wa taifa hilo kutoka pande zote mbili. Rais Alassane Outtara alishinda uchaguzi wa Novemba mwaka jana lakini ghasia zikazuka mara tu baada ya rais aliyekuwepo madarakani Laurent Gbagbo kukataa kuachia madaraka. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 3,000 waliuawa katika ghasia za miezi minne ya kung’ang’ania madaraka. Pia unasema pande zote mbili zilihusika katika ghasia za kivita. Mapema mwezi huu mahakama hiyo ya jinai yenye makao Hague nchini Uholanzi iliagiza uchunguzi ufanywe kubaini ikuwa uhalifu wa kivita ulifanywa. Bwana Ouattara aliapishwa kuongoza taifa hilo baada ya Bw. Gbagbo kukamatwa na kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani.

XS
SM
MD
LG