Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:35

Mahakama Saudi Arabia yamhukumu mwanamke mwanaharakati kifungo cha zaidi ya miaka mitano


Mwanaharakati Loujain al-Hathloul
Mwanaharakati Loujain al-Hathloul

Mahakama moja nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mwanaharakati wa haki za binadamu Loujain al-Hathloul kutumikia kifungo cha karibu miaka sita.

Chombo cha habari cha Sabq chenye uhusiano na serikali kimesema mahakama ya kupambana na ugaidi ya Saudi Arabia imemkuta al-Hathloul na hatia ya uchochezi wa kuleta mabadiliko, akifuata ajenda ya kigeni na kutumia mtandao wa intaneti kuharibu utulivu wa umma.

Al-Hathloul amekuwa jela tangu mwaka 2018 baada ya kukamatwa pamoja na wanawake wengine raia wa Saudi Arabia wasiopungua darzeni moja ambao ni wanaharakati wa haki za binadamu.

Alikuwa anataka kuwepo mageuzi kama vile sheria ya mwanaume kumsimamia mwanamke na kuwaruhusu wanawake haki yao ya kuendesha magari.

Kesi ya mwanamke huyu imekosolewa na wataalam wa haki za binadamu wa UN, makundi ya haki za binadamu na wabunge wa Marekani na Umoja wa Ulaya.

XS
SM
MD
LG