Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 27, 2023 Local time: 22:21

Wizara za Serikali Tanzania kuhamia Dodoma ifikapo September 2016


Rais John Magufuli

Serikali ya Tanzania imetoa agizo kwa watendaji wake muhimu wakiwemo mawaziri kutekeleza azma ya kuhamishia shughuli za serikali makao makuu ya nchi hiyo mkoani Dodoma kutoka jijini Dar es Salaam haraka iwezekanavyo

Agizo la awali la kuhamishia shughuli za serikali makao makuu ya nchi Dodoma, kutokea Dar es salaam, kutekeleza matakwa ya muasisi wa taifa la Tanzania hayati Mwalimu Julius Nyerere, lilitolewa mwishoni mwa wiki na Rais John Magufuli wakati akichukua rasmi uenyekiti wa taifa wa CCM mjini Dodoma.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:39 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, viongozi wakuu wa nchi rais Magufuli na waziri mkuu Kassim Majaliwa wamesisitiza kwamba serikali yao itahamia Dodoma kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya uongozi wao.


Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema atahamia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu na kutaka mawaziri wote waondoke Dar es Salaam kutekeleza agizo hilo.

XS
SM
MD
LG