Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 11:02

Madaktari waliogoma kukiona Tanzania


Picha ya daktari akimuhudumia mgonjwa.

waziri mkuu asema atawafukuza wote kazi endapo wataendelea na mgomo.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ametishia kuwafukuza kazi madaktari wote wanaojihusisha na mgomo nchini Tanzania baada ya kususia kutoa huduma zao na kusababisha vifo kwa wagonjwa.

Jana waziri mkuu alikubali kukutana na madaktari wanaofanya mgomo nchini Tanzania kwa wiki kadhaa sasa, lakini akijikuta peke yake kufuatia madaktari hao kuahidi kutokea na baadae kupuuzia wito huo.

Imeelezwa kuwa hivi sasa maafisa wa muhimbili wamedai kuwepo na hali mbaya katika hospitali hiyo kwa vile madaktari hao wanakwenda kusaini vitabu na kuondoka bila kutoa huduma yoyote. Hali hiyo pia imekumba hospitali nyingine nchini Tanzania kama vile Ocean Road maarufu kwa matibabu ya Saratani jijini dar es salaam, ambapo pia inaelezwa kwamba hakuna huduma yoyote inayotolewa.

Wiki iliyopita maafisa wa Muhimbili walitoa tamko hadharani kudai kwamba hakuna mgomo wowote unaoendelea na shughuli za matibabu zinatolewa kama kawaida.

Madaktari waliamua kugoma baada ya kuitaka Serikali kuwaongeza mishahara na huduma bora madai ambayo yametupiliwa mbali.

Mpaka sasa bado idadi kamili ya watu waliokufa kufuatia mgomo huo bado haijatolewa.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG