Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:52

Madaktari wa msaada washambuliwa Somalia


Madaktari wa kutoa huduma za afya nchini Somalia washambuliwa Jumatano mjini Mogadishu
Madaktari wa kutoa huduma za afya nchini Somalia washambuliwa Jumatano mjini Mogadishu
Watu wenye silaha nchini Somalia wameshambulia msafara uliowabeba madaktari kuelekea hospitali moja karibu na mji mkuu Mogadishu na kuwauwa watu sita wakiwemo raia watatu wa Syria.

Shambulizi hilo la kushtukiza limetokea Jumatano kwenye barabara moja ambayo inaunganisha Mogadishu kuelekea Afgoye. Mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika-VOA- mjini Mogadishu anasema daktari mwingine raia wa Syria alijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Afgoye ni ngome ya zamani ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab wenye uhusiano na al-Qaida ambao walikana kuhusika na mashambulizi hayo. Kundi la al-Shabab liliwahi kudhibiti maeneo mengi ya mji mkuu Somalia lakini kundi hilo lilifukuzwa kutoka Mogadishu na miji mingine mikubwa na walinda amani wa Umoja wa Afrika.

Kundi la Al-Shabab linaendelea kufanya mashambulizi ikiwemo moja kwenye kituo cha polisi katika mji wa Beledweyne mwezi uliopita ambalo liliuwa zaidi ya watu 20.
XS
SM
MD
LG