Shirika la afya duniani (WHO) limefunga moja ya maabara zake za uchunguzi wa Ebola nchini Sierra Leone baada ya mfanyakazi mmoja kwenye maabara hiyo kuambukizwa na virusi vya Ebola.
WHO ilisema Jumanne kwamba inawaondoa wafanyakazi wake kutoka maabara ya Kailahun ambayo ni moja kati ya maabara mbili pekee zilizopo nchini Sierra Leone baada ya mtaalamu wa magonjwa yanayoambukiza kutoka Senegal, kuambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha maafa.
Hatua hiyo itadumaza juhudi za kupambana na mlipuko mbaya wa ugonjwa huo kuwahi kutokea nchini humo.Ugonjwa wa Ebola umeuwa zaidi ya watu 1,400 na kuambukiza 2,600 katika mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi tangu mlipuko huo ulipoanza mwezi Machi.