Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 20:42

Rais Sirleaf wa Liberia atarajiwa kushinda


Raia wa Liberia akipiga kura katika moja ya vituo vya kupigia kura nchini humo

Upinzani nchini Liberia umesusia kushiriki duru ya pili ya uchaguzi wa urais na kutoa nafasi ya ushindi kwa Rais wa sasa Ellen Johnson Sirleaf

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf anatarajiwa kushinda tena uchaguzi wa rais katika duru ya pili ya upigaji kura ambao umesusiwa na upinzani na kupelekea mapambano makali yaliyosababisha vifo kati ya polisi na waandamanaji.

Waziri wa zamani wa sheria Winston Tubman, mpinzani mkuu kwenye kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi wa Jumanne amewataka wafuasi wake kususia upigaji kura kwa sababu shutuma za kuwepo wizi wa kura kwenye uchaguzi huo ambao unampendelea bibi. Sirleaf.

Ghasia zilizuka katika mji mkuu wa Monrovia, Jumatatu nje ya makao makuu ya chama cha Tubman cha Congress for Democratic Change CDC, ambapo ghasia kati ya polisi wa Liberia na wafuasi wa upinzani zilisababisha kifo cha mtu mmoja.

Serikali ya Liberia imesema upigaji kura utaendelea licha ya ghasia hizo. Na Mwandishi wa sauti ya Amerika, mjini Monrovia, Scott Stearns, anasema idadi ya wapigakura waliojitokeza imekua ndogo ikiwa ni pamoja na kituo kituo kimoja kilichokua na mistari mirefu wakati wa duru ya kwanza ya upigaji kura iliyofanyika mwezi uliopita.

Polisi walifunga vituo vitatu vya Radio usiku kucha ikiwemo kituo kimoja kinachomilikiwa na mgombea mwenza wa bwana. Tubman, George Weah.
Msemaji wa polisi nchini humo, George Bardue, aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba polisi wanatekeleza amri ya mahakama ya kuvifunga vituo hivyo baada ya ghasia za Jumatatu.

Lori moja la polisi wa Liberia liliwasili kwenye makao makuu ya CDC Jumanne, lakini walikumbana na wafuasi wa CDC ambao walitoka nje na kupiga kelele “hatutaki polisi”. Polisi waliondoka baada ya kutakiwa kufanya hivyo na walinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao wanalilinda eneo hilo.

Rais wa Marekani Barack Obama alisema jumuiya ya kimataifa itawalaumu wale ambao wanachagua kuzuia utaratibu wa demokrasia nchini Liberia. Pia aliyahamasisha majeshi ya usalama ya Liberia kutumia nguvu za kawaida na kuruhusu maandamano ya amani.

Wafuatiliaji wa uchaguzi walisema duru ya kwanza ya upigaji kura kwa ujumla ilikuwa huru na haki.

XS
SM
MD
LG