Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:51
VOA Direct Packages

Kundi la Islamic State ladai kuhusika kwenye mauaji ya wanajeshi, Burkina Faso


Wanajeshi wa Burkina Faso wakiwa kwenye mafunzo ya kukabiliana na magaidi.

Kundi la Islamic State limedai kuhusika kwenye mauaji ya zaidi ya wanajeshi 70 na kujeruhi wengine kadhaa na kutekwa nyara watu watano wakati wa shambulizi  la kushtukiza dhidi ya msafara wa kijeshi kaskazini mwa Burkina Faso.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, taarifa iliyochapishwa Ijumaa na chombo cha habari cha kundi hilo cha Amaq, imesema kwamba kundi hilo liliushambulia msafara uliokuwa unajaribu kusonga mbele kwenda kwenye maeneo wanayoyadhbiti karibu wa Deou katika jimbo la Oudalan huko Sahel.

Ripoti zimeongeza kuwa wanajeshi hao walipokonywa silaha, pamoja na kufukuzwa kwa maili kadhaa ndani ya jangwa. Picha zilizotolewa na kundi hilo zimeonyesha miili 54 ya wanajeshi waliovalia sare, zaidi ya bunduki 50 walizopora, pamoja na wanajeshi watano waliotekwa nyara.

Shambulizi hilo limefanyika wiki moja baada ya jingine kwenye eneo hilo na siku kadhaa baada ya lile ambalo lilifanyika kwenye mji wa Tin Akoff ambako wakazi na mashirika ya kiraia wanasema kwamba darzeni ya wanajeshi pamoja na raia waliuwawa, baada ya shambulizi dhidi ya kituo kimoja cha kijeshi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG