Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:13

Kenya yagundua mafuta Turkana


Eneo la Turkana kulikogunduliwa mafuta - Kenya
Eneo la Turkana kulikogunduliwa mafuta - Kenya

Kampuni ya Uingereza kwa jina Tullow ilisema iligundua mafuta hayo kwneye kina cha mita 20 chini ya ardhi.

Rais wa Kenya Mwai Kibaki ametangaza Jumatatu kuwa mafuta yamegunduliwa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya lakini akatahadharisha kuwa itachukua miaka kabla ya uzalishaji wa mafuta hayo kuanza.

Rais Kibaki alisema ugunduzi wa mafuta hayo katika eneo la Turkana ni hatua muhimu lakini njia ndefu kufikia mwanzo wa uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Kampuni ya Uingereza kwa jina Tullow ilisema iligundua mafuta hayo kwneye kina cha mita 20 chini ya ardhi.

Msemaji wa kampuni hiyo George Cazenove amesema ugunduzi huo ni tukio muhimu lakini anatahadahrisha kuwa hatua zitakazofuata hadi kuyazalisha mafuta hayo itakuwa kazi kubwa.

Kampuni ya Tullow inasema itaendelea kuchimba kisima hicho kufikia mita elfu 2,700 ili kubaini ikiwa kuna mafuta zaidi.

Katika taarifa kampuni hiyo imesema mafuta yaliyogunduliwa katika eneo la Turkana yanafanana kwa uzito na yale yaliyogunduliwa nchini Uganda na kwmaba hilo jambo muhimu pia.

XS
SM
MD
LG