Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:15

Katibu Mkuu wa NATO afanya ziara ya kushtukiza Ukraine


Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy baada ya kuwasili Kyiv

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg Alhamisi amefanya ziara ya kushtukiza  nchini Ukraine, ikiwa ni ya kwanza  nchini humo tangu uvamizi wa Russia, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Stoltenberg ametembelea kumbukumbu ya wanajeshi waliopoteza maisha yao, na kukagua vifaa vya kijeshi vya Russia vilivyoharibiwa, ambavyo vinaonyeshwa katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Stoltenberg amekuwa akiunga mkono, mara kwa mara, wanachama wa NATO wanaotoa silaha kuvisaidia vikosi vya Ukraine, na ameshuhudia muungano huo ukikua, baada ya Finland kujiunga nao mwezi huu, kama njia ya kujibu uvamizi huo.

Pia ombi kama hilo kutoka kwa majirani wa Finland, Sweden, limeidhinishwa na wanachama wote wa NATO, isipokuwa tu Hungary na Uturuki.

Wanachama wa NATO, Denmark na Uholanzi, walitangaza Alhamisi kuwa wanashirikiana kununua na kukarabati vifaru 14 vya Leopard 2-A4, vilivyotolewa kwa Ukraine. Wizara ya Ulinzi ya Uholanzi na Denmark ilisema vifaru hivyo vitakuwa tayari kuwasilishwa kwa vikosi vya Ukraine mapema mwaka ujao.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg asema: “Hatujui ni lini vita hivi itamalizika , lakini tunajua uchokozi wa Russia ni sumu ambayo lazima isitishwe. Tumekubaliana kuhusu umuhimu wa makubaliano endelevu ya amani, na ninakaribisha kwa nguvu mpango wa amani wa Zelensky. Lazima tuendelee kuimarisha vikosi vya kijeshi vya ukraine na lazima tuhakikishe kwamba utaratibu wenye nguvu upo kwa ajili ya usalama wa ukraine.”

Wakati huohuo msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kwamba kuizuia Ukraine kujiunga na NATO bado ni moja ya malengo ya operesheni maalumu za kijeshi za Moscow, amesema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.

XS
SM
MD
LG