Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:38

Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa aonya kuwa hali kaskazini mwa Ethiopia inazidi kudorora


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza wakati wa mahojiano kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Januari 20, 2022, New York. AP.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza wakati wa mahojiano kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Januari 20, 2022, New York. AP.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alionya Jumatatu kwamba hali ya kaskazini mwa Ethiopia "inazidi kudorora" na haoni suluhu ya kijeshi ikifanikiwa kwenye mzozo huo.

Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono Umoja wa Afrika kwa kila njia ili kumaliza jinamizi hili kwa watu wa Ethiopia, alisema. Tunahitaji kuanzishwa tena kwa haraka kwa mazungumzo kuelekea suluhu ya kisiasa yenye ufanisi na ya kudumu aliongeza .

“Vurugu na uharibifu umefikia viwango vya kutisha; mfumo wa kijamii unasambaratika,” Antonio Guterres aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Akiongeza kwamba "Uhasama katika eneo la Tigray nchini Ethiopia lazima ukomeshwe sasa ikiwa ni pamoja na kuondoka mara moja na kujiondoa kwa wanajeshi wa Eritrea kutoka Ethiopia."

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema ni lazima jumuiya ya kimataifa iungane pamoja ili kumaliza mzozo huo uliodumu kwa takriban miaka miwili, ambao umeua na kujeruhi maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni kwenye ukingo wa njaa.

XS
SM
MD
LG