Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini inataka hali ya dharura ya kitaifa kutangazwa sawa na ile iliyotangazwa kukabiliana na janga la Covid 19 ili kusaidia kumaliza hali ya ukosefu wa umeme.
Katibu Mkuu wa ANC Fikile Mbalula aliwaambia waandishi wa habari leo Jumanne kwamba kamati kuu ya utendaji ya ANC baada ya kukutana imeitaka kamati ya kukabiliana na mzozo wa nishati inayomshauri Rais Cyril Ramaphosa kuharakisha kazi yake.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambae hakuhudhuria mkutano wa Jopo la Kiuchumi Duniani huko Davos mwezi huu kwa sababu ya ukosefu wa umeme, anatarajiwa kutangaza hatua mpya za kuongeza huduma za umeme wakati wa hotuba yake juu ya hali ya taifa hapo Februari 9.