Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:07

Jihad Azour ameteuliwa na vyama tofauti vya Lebanon kuwania urais nchini humo


Jihad Azour, mkurugenzi wa Mashariki ya Kati na Asia ya Kati katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)

Lebanon haijawahi kuwa na mkuu wa taifa tangu muhula wa rais Michel Aoun ulipomalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba na kuzidisha hali ya kukwama zaidi kazi za idara na wizara katika nchi ambayo inashuhudia mojawapo ya mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi duniani imekuwa ikizorota kwa miaka mingi

Vyama vya upinzani dhaifu vya Lebanon pamoja na vyama huru na vikuu vya Kikristo vimesema Jumapili kuwa vimemteua afisa wa IMF, Jihad Azour kuwania kinyang’anyiro cha urais dhidi ya mgombea anayeungwa mkono na Hezbollah Suleiman Franjieh.

Mkutano wa vyama uliidhinisha uteuzi wa Azour, ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa Mashariki ya Kati na Asia ya Kati katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na pia waziri wa zamani wa fedha wa Lebanon. Lebanon haijawahi kuwa na mkuu wa taifa tangu muhula wa rais Michel Aoun ulipomalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba na kuzidisha hali ya kukwama zaidi kazi za idara na wizara katika nchi ambayo inashuhudia mojawapo ya mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi duniani imekuwa ikizorota kwa miaka mingi.

Hezbollah, kundi lenye nguvu kubwa za kisiasa katika nchi hiyo, na mshirika wake kundi la Kishia la Amal, walikuwa wamemuunga mkono Franjieh, mwenye umri wa miaka 56 mrithi wa utawala wa zamani wa kisiasa wa Kikristo wa Lebanon, na mshirika wa Rais wa Syria Bashar al-Assad mwenye uhusiano mkubwa na taasisi ya kisiasa ya utawala huko Damascus.

Forum

XS
SM
MD
LG