Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 07, 2025 Local time: 12:09

Jeshi la Sudan lafanikiwa dhidi ya kundi ya RSF


Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan alipoitembelea kambi ya jeshi ya Flamingo iliyoko Port Sudan, Agosti 28, 2023. Picha na AFP.
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan alipoitembelea kambi ya jeshi ya Flamingo iliyoko Port Sudan, Agosti 28, 2023. Picha na AFP.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba Kundi la wanamgambo la Sudan -RSF limeanza kupoteza nguvu dhidi ya jeshi la taifa kutokana na makosa ya mikakati, ugomvi wa ndani kati ya viongozi wake na kupungua vifaa.

Jeshi la taifa limepata mafanikio na kuonekana kugeuza hali ya mambo katika vita vilivyodumu kwa takriban miaka miwili ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kuwakosesha makazi wengine elfu 12.

Mwezi uliopita jeshi lilipata nguvu na kupita Katikati mwa Sudan kwa kukomboa mji wa Al- Jazira wa Wad Madani kabla ya kujielekeza zaidi Khartoum.

Ndani ya wiki mbili lilisambaratisha RSF iliyokuwa imezingira kambi muhimu za kijeshi Khartoum ikiwemo makao makuu ya jeshi na kuchukua udhibiti wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha AL-Jaili kikubwa zaidi nchini humo kaskazini mwa mji mkuu.

Wakati huo huo Jumatatu mapigano makali yametokea kusini na magharibi mwa Sudan ambako takriban watu 65 wamekufa na wengine 130 wamejeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG