Jeshi la Israel limesema Jumanne kuwa vikosi vyake vilimuua mtu mmoja aliyekuwa na silaha katika Ukingo wa Magharibi ambaye aliwafyatulia risasi wanajeshi. Jeshi hilo limesema majibizano ya risasi yalifanyika kwenye kituo cha ukaguzi katika kijiji cha Tayasir.
Maafisa wa huduma za dharura wa Israel wamesema watu wasiopungua sita wamejeruhiwa wakiwemo wanajeshi wawili. Katika wiki za hivi karibuni jeshi la Israel limekuwa likifanya operesheni katika eneo hilo hasa karibu na Jenin ambapo jeshi linasema linalenga kuzuia ugaidi.
Jeshi lilisema Jumapili kuwa limewaua wanamgambo angalau 50 tangu kuanza kwa operesheni hiyo wiki mbili zilizopita wakati maafisa wa afya wa Palestina walisema vikosi vya Israel vimewaua watu 70 katika Ukingo wa Magharibi tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Ghasia katika Ukingo wa Magharibi ziliongezeka kufuatia shambulio la Oktoba 2023 la Hamas dhidi ya Israel, na mashambulizi ya Israel dhidi ya kundi la kigaidi lililotangazwa na Marekani katika Ukanda wa Gaza.
Forum