Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 05:04

Israel na wanamgambo wa Palestina wakubaliana kusitisha mapigano


Mwanaume wa Kipalestina amembeba bintiye baada ya kuhama nyumba yake wakati wa mashambulizi ya anga ya Israel mjini Gaza, Agosti 7, 2022. Picha ya AFP

Misri imesadia katika upatanishi wa kuleta sitisho la mapigano huko Gaza kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina, Islamic Jihad.

Utekelezaji wa makubaliano hayo ulikuwa unatarajiwa kuanza saa tano na nusu usiku majira ya huko. Afisa wa idara ya ujasusi ya Mistri ameiambia Associated Press kwamba pande hizo mbili zimeridhia makubaliano hayo.

Sitisho hilo la mapigano litamaliza mapigano mabaya katika ukanda wa Gaza tangu vita vya siku 11 vya mwaka jana kati ya jeshi la Israel na kundi la Hamas, kulingana na ripoti.

Wizara ya afya huko Gaza imesema watu 31 waliuawawa katika mashambulizi ya anga ya Israel, wakiwemo watoto sita, huku Israel ikisema haikuhusika na vifo vya watu 9 kati ya waliouawa.

Mapigano ya hivi sasa yalianza pale Israel ilipomkamata afisa mwandamizi wa kundi la Islamic Jihad wiki iliyopita na kijana Mpalestina wa umri wa miaka 17 kuuawa. Islamic Jihad yenye ngome zake huko Gaza, ilitishia kulipiza kisasi.

Siku ya Ijumaa, Israel ilifanya mashambulizi ya anga huko Gaza, na kumua kamanda wa kundi la Islamic Jihad.

Tangu wakati huo, Islamic Jihad ilirusha takriban makombora 600, ambayo mengi yalidunguliwa na vifaa vya kijeshi vya Israel, maarufu Iron Dome system.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG